Kendrick
Lamar athibitisha uhusiano wake Na mpenzi wake wa zamani ambaye alikuwa aki toka
naye kimapenzi tangu walipokuwa high school lakini hivi sasa inasemekana
wanampango wa kuoana rasmi.
Kendrick Lamar's ambaye hivi sasa album yake ya To Pimp a Butterfly inaendelea kusumbua kwenye Billboard chati 200 kwa zaidi ya wiki ya pili sasa , lakini
rapper huyo kutoka mjini Compton mapema jana alizungumzia kuhusiana na uhusiano
wake na mkewe mtaarajiwa Whitney Alford
kwamba si habari mbaya mahusiano
yao yakiwekwa bayana nafikiri ni habari njema
katika maisha yangu . Kendrick Lamar‘s
alijikuta amezama kwenye penzi la mtoto Whitney Alford msichana ambaye walisoma
wote enzi hizo tangu wakiwa high school.
Kendrick amethibitisha hayo alipokuwa
akihojiwa na kituo cha radio kwenye kipindi cha breakfast club jana asubuhi jijini New York ,
mtangazaji wa kipindi hicho alimuuliza swali Kendrick lamar jee ni kweli kuna uhusiano wowote uliopo kati
yake yeye na Whitney Alford akajibu ni kweli sio siri tena nafikiri unafahamu
hilo, Kendrick lamar akamaliza kwa kusema “I'm loyal to the soil” Na hatimaye
siku ya mwisho tunataka watu wafahamu kwamba kumbe tunaishi na watu wenye
malengo haijalishi ni mwanaume au ni mwanamke jamii yote inayokuzunguka
inapaswa kufahamu hilo.
Lakini ikumbukwe kuwa Kendrick amewahi
kuhojiwa mwezi January na mmoja wanao host kipindi cha Billboard na kuulizwa
swali kuhusu Whitney Alford je ni mpenzi wake au raha? kwa bahati mbaya au
nzuri alikataa kata kata alisema ni rafiki yangu wakike hakuna kingine zaidi ya hicho. Naweza sema ni rafiki yangu tulifahamiana
tukiwa wote shuleni kwa namna nyingine naweza kumuita ni zaidi ya rafiki.
Jina lake halisi
anaitwa Kendrick Lamar Duckworth alizaliwa tarehe 17 mwezi june mwaka 1987
anafahamika kama Kendrick Lamar,
ni msanii wa miondoko ya HipHop akitokea mjini Compton,
jijini California. Mwaka 2004, Lamar alisaini mkataba na kuwa
chini ya label ya Top
Dawg Entertainment (TDE). Baadaye tena Lamar alisaini mkataba na studio
mbili tofauti hii ilikuwa mwaka 2012, pale ambapo aliingia rasmi kwenye studio
za Aftermath
na Interscope
Records.
Ukiachana na kazi yake ya mziki, Lamar amewahi kuwa mwanachama wa kundi la Black Hippy
na baadaye kundi hilo kuitwa Super
Group kipindi hicho
akiwa baado mdogo kundi hilo lilifahamika sana na kujipatia umaarufu kote
duniani.
kwa maelezo yake anasema Super
Group ni kundi ambalo
lina wasanii wa hiphop wanaotokea kwenye
ukanda wa Magharibi Na Kusini Mwa Los Angeles wasanii wote walikuwa chini ya
label ya Top
Dawg Entertainment {TDE} hakuwa pekee yake bali alikuwa na
wasanii wenzake kama vile Schoolboy Q, Jay Rock,
na Ab-Soul.
Umaarufu wake na kazi zake ndiyo zilizomfanya akutane na wasanii
wakongwe wa Hip Hop kutoka nchini marekani na hatimaye aliweza kufanya nao kazi
mbali mbali miongoni wa wasanii hao
ni Dr. Dre,
The Game,
Eminem,
Drake,
Young Jeezy,
Talib Kweli,
Busta Rhymes,
E-40,
Warren G,
na Lil Wayne
ndipo alipoanza kuona soko la muziki wa Hip
Hop jinsi lilivyo na unatakiwa kufanya nini ili uweze kuyafikia malengo yako.
kingine kipya fahamu ya kwamba album
iliyomtoa Lamar's kwenye mziki ni ile ya , Good
Kid, M.A.A.D City, aliyoiachia rasmi October mwaka 2012 na kusambazwa duniani kote.
Album hiyo ilikuwa na zile nyimbo kali ambazo zilipata nafasi ya kuingia kwenye
orodha ya Top 40
hits miongoni mwa nyimbo hizo ni "Swimming
Pools (Drank)", "Bitch,
Don't Kill My Vibe", na ile ya "Poetic
Justice". Baada ya kuachia album hiyo ilipewa shavu na
kushika nafasi ya pili kwenye US Billboard 200
chart na baadaye iliweza kuthibitishwa na hatimaye kuwa miongoni mwa album ambazo zimeingia kwenye
orodha ya Platinum kwa mjibu wa (RIAA).
Album yake ya kwanza kutoka ilikuwa ni Youngest Head Nigga In Charge
mwaka 2003, ikifuatiwa na C4 mwaka 2009, ikaja Overly Dedicated mwaka 2010,
Section mwaka 2011 lakini zilizo hit na kutikisa vituo vya luninga na vituo vya
radio ni ile ya Good Kid M.A.A.D City ya mwaka 2012 na hii mpya ya To Pimp A
Butterfly aliyoitoa mapema mwezi march mwaka huu wa 2015.
Mapema mwaka 2013 kituo kikubwa na maarufu cha luninga cha MTV Base kilimtunuku Kendrick Lamar kuwa msanii
chipukisi namba moja kwenye mziki wa hip hop na kwenye
tuzo za MTV orodha ya awali inadhihirisha Lamar amepokea jumla ya tuzo saba za Grammy
katika kinyang’anyiro hicho akiwa kama
Best
New Artist, Album
of the Year na Best
Rap Song hiyo ilikuwa mwaka 2014. Na mwaka 2015
aliweza kushinda tuzo 2 ambazo ni A Best
Rap Performance na Best
Rap Song for his single.
No comments:
Post a Comment