Thursday, December 11, 2014

Tume ya Taifa ya uchaguzi Kujaribu Mfumo Wa Biometric Voter Registration BVR

Tume ya Taifa ya uchaguzi NEC inatarajia kuanza kufanya majaribio ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura kwa kutumia mfumo mpya wa biometric voter registration BVR katika majimbo matatu ya uchaguzi ambayo ni Kawe, katika manispaa ya Kinondoni, Kilombero Mkoa wa Morogoro na wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi.







Zoezi hilo la majaribio linatarajiwa kuanza Disemba 15 mwaka huu hadi Disemba 24 mwaka huu, huku vyama vya siasa vikipewa fursa ya kuweka mawakala wao katika vituo hivyo ili kushuhudiaa namna uandikishaji utakavyofanyika.



Akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa Jijini Dar es salaam Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid alisema, tume imepokea kiasi cha fedha, pamoja na mashine za BVR 107 huku nyingine zikitarajiwa kupokelewa ndani ya wiki hii.
Aidha Jaji Hamid alisema kuwa zoezi la majaribio litakwenda sambamba na zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura katika mikoa yote Tanzania isipokuwa katika mikoa ya Zanzibar, Dar es salaam, Pwani na Morogoro.


Kwa upande wa baadhi ya wanasiasa kutoka vyama vya CHADEMA na ADC  wameonyesha wasiwasi katika zoezi hilo pamoja na kuitaka tume kutoshirikisha Jeshi la wananchi JWTZ kwani zoezi hilo litakosa sura ya kidemokrasia.

No comments:

Post a Comment