Friday, July 18, 2014

Nelson Rolihlahla Mandela alizaliwa July 18, 1918 Mvezo, jimbo la Cape town na kufariki December 5 mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 95 huko nchini afrika ya kusini, Johannesburg.








 Atakumbukwa kwa mema aliyowafanyia wananchi wa afrika ya kusini na duniani kote kwa kutetea haki za kibinadamu , ubaguzi wa rangi ambao kwa kiasi kikubwa lilikuwa ni janga kubwa mno kwenye taifa hilo.




 Alishika wadhifa wa kuwa rais wa kwanza nchini Afrika ya Kusini mwaka 1994 mpaka 1999 ni mwanasiasa, mwanamapinduzi, mwanafasafa, lakini pia amewahi kuwa mtendaji mkuu wa kwanza wa afrika ya kusini na alichaguliwa kuwa Rais kwa uchaguzi sahihi tena wa kidemokrasia na hakuna aliyepinga kuhusu hilo.



 Serikali yake ilijikita zaidi kwenye masuala ya kutokomeza umasikini, ubaguzi wa rangi, mambo ya urasimu. Hivi hapa ni baadhi ya Vyama vya siasa ambavyo amewahi kuvitumikia enzi za uhai wake chama cha siasa cha taifa la Afrika ya Kusini na ujamaa wa kidemokrasia alikitumikia akiwa kama Rais wa chama cha (ANC) yaani African National Congress kuanzia mwaka 1991 hadi 1997 Nelson Mandela ambaye maisha yake alijitoa muhanga kwa kila jambo pale ambapo aliamua kupigania huru wa nchi yake huku akiwa na nia njema tuu lakini pia  sheria,  misingi ya utu wa kibinadamu ifuatwe. Lakini pia aliwahi kushika wadhifa wa kuwa katibu mkuu wa (NAM) yaani Non-Aligned Movement kuanzia mwaka 1998 hadi 1999.





Siku hii ya leo ni nafasi pekee ya kuchukua atua kwa vitendo kwa kufanya uombolezaji kutokana na jitahada zake alizozifanya enzi za uhai wake ikiwa pamoja na kukubari mabadiliko aliyoyafanya na wengi kuvutiwa karibu kila pembe ya dunia,tumia angalau dakika kadhaa kuhamasisha ulimwengu na kuwaombea/kuwasihi wengine .




Alikulia kwenye kijiji cha Xhosa na alipata bahati ya kuzaliwa katika familia bora ambayo waliita kwa jina la Thembu, Mandela alipata fursa ya kusoma chuo kikuu cha  Fort Hare  na baadaye alijiunga na chuo kikuu cha  Witwatersrand, wakati huo alikuwa anasomea sheria .Aliishi  Johannesburg, alianza kujishugurisha na siasa za kikoloni , na ndipo alipopata fursa ya kujiunga na chama cha ANC na kuwa ni miongoni mwa mwanachama ambaye aliweza kuwa muasisi wa kundi la Youth League . Baada ya chama cha  ASANP kushika madaraka mwaka 1948 kilikuwa na nguvu mno , mzee Nelson Mandela alianza kupoteza matumaini akidhani ya kwamba hapo baadaye chama chake cha ANC kamwe hakitoweza kuja kushika wadhifa wowote ule nchini humo lakini hakukata tamaa mwanzoni mwa mwaka 1952 alianzisha kampeni zake  baadaye aliteuliwa na wanachama wake kugombea baadhi ya nyadhifa  kupitia moja la shirika lisilo la kiserikali la Transvaal na alitumikia mpaka mwaka  1955. Alifanya kazi akiwa kama mwanasheria, alianza kuzipitia upya baadhi ya shughuri ambazo zilikuwa zikifanywa na ANC.


Mandela alitumikia kifungo cha jela kwa mda wa miaka 27 miongoni mwa magereza ambayo amewahi kuyatumikia ni  Robben Island, baadaye huko Pollsmoor  na Victor Verster .  Alitoka jela mwaka 1990 wakati ule ambao nchi ya afrika ya kusini ilikuwa katika mgogoro mkubwa sana . 


Mandela baada ya kutoka jela aliungana na mtu wake wa karibu ambaye alikuwa ni Rais pia ndugu  F. W. de Klerk ili kukomesha vitendo vilivyokuwa vinaenda kinyume na vile anavyoishi binadamu,kuimarisha hali ya usalama wa taifa lao na hatimaye kuitisha uchaguzi mwaka  1994.



Nafasi iliyomfanya asimame kidedea kuwania urais na hatimaye kushinda kwa kishindo kuwa Rais wa kwanza mweusi nchini Afrika ya Kusini na hakuna aliyeamini mpaka pale walipochapisha kwenye baadhi ya magazeti,vituo vya redio kutangaza na vituo vya luninga kurusha moja kwa moja kilichokuwa kinaendelea kwenye uchaguzi huo.






 
Alioa mitara waswahili wanasema hivyo, lakini wenzetu wazungu wanaita “monogamy” Mke wake wa kwanza anaitwa Evelyn Ntoko Mase (ambaye waliishi naye kuanzia mwaka 1944 na walitarakiana mwaka 1957) wapili ni  Winnie Madikizela (ambaye waliishi naye kuanzia mwaka  1958 na walitarakiana mwaka  1996) watatu na wa mwisho alikuwa ni  Graça Machel (ambaye waliishi naye kuanzia mwaka 1998–2013 mpaka umauti unamkuta)


Nelson  Mandela mpaka anafariki ameacha watoto sita tuu ambao ni :
Thembekile Mandela,Makaziwe Mandela,Makgatho Mandela,Makaziwe Mandela, Zenani Mandela na Zindziswa Mandela







Akiendelea na majukumu yake ya kila siku kama rais muasisi wa taifa hilo aliweza tena kuanzisha baraza la kutetea ukombozi wa sera ya uchumi , utawala wake/uongozi wake uliwenza  kutanguliza upya na uanzishwaji wa sheria ya aridhi ambapo kila mwananchi alipata nafasi ya kumilikishwa aridhi kupitia sheria hiyo, si hivyo tuu walianzisha tena sheria  ya kuzuia na kumbambana na rushwa, sheria ya kuhakikisha kila mwananchi anapata elimu bora kujengwaa kwa kasi vyuo vikuu,shule za sekondari,vyuo vya ufundi na shule za awali, huduma bora za afya kama vile upatikanaji wa hospitali,vituo vya zahanati na kadhalika,upatikanaji wa lishe bora,ujenzi wa miundo mbinu ya barabara,reli,anga na majini. Ujenzi wa viwanda vikubwa uwekezaji wenye manufaa kwa taifa husika.






No comments:

Post a Comment